×

Video: Watu 9 Wanusurika Kifo Baada ya Lori la Mafuta Kulipuka Morogoro

Watu tisa, wakiwemo askari watatu—wawili wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na mmoja wa Jeshi la Polisi—wamenusurika kifo kufuatia mlipuko wa lori la mafuta uliotokea katika eneo la Doma, kwenye barabara kuu ya Morogoro–Iringa.

Tukio hilo limetokea wakati wahusika walipokuwa wakifanya juhudi za kuhamisha mafuta kutoka kwenye lori hilo lililokuwa limepinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, SSF Shabani Marugujo, amesema majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu, huku baadhi yao wakihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kuungua sehemu mbalimbali za miili yao.

Leave a Comment