Milioni. 500/- Zachangwa na Nmb Kupanua Huduma za Hospitali ya Benjamin Mkapa
Global Publishers April 17, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu (wa pili kulia), akishuhudia makabidhiano ya mfano wa hundi ya Sh. Milioni 250 kati ya Mkurugenzi wa Uhusiano kwa Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano wa NMB, Innocent Yonazi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital
BENKI ya NMB imeahidi kutoa Sh. milioni 500 kwa kipindi cha miaka miwili kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), kusaidia upanuzi wa huduma za upandikizaji figo na uboho ili kuimarisha huduma za afya za kibingwa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya NMB, Mkurugenzi wa Uhusiano kwa Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano, Innocent Yonazi, alisema mchango huo unaonesha dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kuunga mkono vipaumbele vya maendeleo ya taifa, hususan katika sekta ya afya.Alisema NMB imeendelea kuelekeza sehemu ya faida yake kwenye shughuli za uwajibikaji kwa jamii, huku afya ikiwa miongoni mwa maeneo ya kipaumbele.Ahadi hiyo ilitangazwa jana wakati wa hafla ya uchangishaji fedha iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Sh. milioni 250 zilikabidhiwa kama sehemu ya utekelezaji msaada huo wa miaka miwili.Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, alisema uwekezaji katika huduma maalum za matibabu ni muhimu kwa kuwa unasaidia kupunguza gharama kubwa za kuwapeleka Watanzania nje ya nchi kutafuta tiba hizo.Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof. Abel Makubi, alisema msaada huo utasaidia kuongeza uwezo wa hospitali kutoa huduma hizo muhimu kwa Watanzania wengi zaidi, hasa wasioweza kumudu gharama za matibabu ya kibingwa.Hatua hiyo pia inatajwa kuwa chachu ya kupunguza utegemezi wa rufani za matibabu nje ya nchi, huku ikiimarisha uwezo wa ndani wa Tanzania katika huduma za kibingwa zenye kugusa maisha ya wananchi wengi.