
Simba imetinga hatua ya fainali Muungano Cup 2026 kwa ushindi wa magoli 3-0 Mlandege FC Aprili 29 katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Simba wameonyesha ubora mkubwa magoli yakifungwa na Mwalimu (63’), Oura (76’), na Maema (89’). Ushindi huo unawapeleka moja kwa moja kwenye fainali dhidi ya Yanga Aprili 29, 2026.
Hii inamaanisha mashabiki watapata burudani ya hali ya juu kwa michezo miwili mfululizo:
- Aprili 29, 2026 – Fainali ya Kombe la Muungano Cup 2026
- Mei 3, 2026 – Mechi ya NBC Premier League
Kwa hali ilivyo sasa, Simba wanaonekana kuwa kwenye form nzuri, lakini dabi dhidi ya Yanga huwa haina matokeo ya kutabirika kirahisi historia inaonyesha timu yoyote inaweza kushinda siku hiyo.