
Mfanyabiashara mjane, Fatuma Nassoro, mkazi wa Kaliua mkoani Tabora, amepoteza zaidi ya shilingi milioni 40 baada ya kutapeliwa kwa njia ya simu na watu waliojifanya wahudumu wa kampuni ya mawasiliano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao, amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea kubaini mtandao mzima wa uhalifu huo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa makini wanapopokea simu au ujumbe kutoka kwa watu wasiojulikana, hususan wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa taasisi mbalimbali, ili kujikinga dhidi ya matukio ya utapeli.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.