
AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa kuna raha kubwa kupata ubingwa kwa kumfunga mpinzani ambaye ni msumbufu kwa muda mrefu.
Aprili 29, 2026 Yanga SC 0-1 Simba SC katika mchezo wa fainali Muungano Cup, Uwanja wa New Amaan Complex huku mfungaji akiwa ni Seleman Mwalimu dakika ya 124 kwa mkwaju wa penati iliyosababishwa na Clatous Chama mara baada ya kuchezewa faulo na Edmund John ndani ya 18.
Ahmed amesema: “Kuna raha kutwaa ubingwa mbele ya mtani sio ubingwa tu na raha ni kubwa ukizingatia kwa muda mrefu tulikuwa hatujapata matokeo mbele yao tumefurahi sana na tunaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo.
“Kazi bado inaendelea kwa kuwa mwisho wa mchezo wa leo kuna mechi nyingine ambazo zipo mbele yetu. Tumefanikisha malengo yetu kwenye Muungano Cup bado kuna ligi hivyo furaha inaendelea lakini sio kwa kiasi kikubwa kwa sasa,”.
Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa Muungano Cup walikuwa ni Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves.
Simba SC imetwaa taji hilo huku Kocha Mkuu, Steve Berkar akitwaa tuzo ya kocha bora wa mashindano ya Muungano Cup 2026.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.