×

Beyoncé Ang’ara Met Gala 2026 Arudi Kwa Kishindo Baada Ya Miaka 10

Msanii maarufu wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Beyonce

Tamasha la mitindo la Met Gala limefanyika kwa kishindo usiku wa kuamkia leo Mei 5, 2026 huku mastaa mbalimbali wakionyesha ubunifu mkubwa kwenye mavazi yao.

Msanii maarufu wa muziki wa R&B wa nchini Marekani, Beyonce ameibua gumzo baada ya kuonekana akiwa amevalia vazi la kifahari lililopambwa kwa shanga na kuongezewa joho kubwa la manyoya baada ya miaka 10.

Aliongozana na binti yake, Blue Ivy Carter, aliyejitokeza kwa mara ya kwanza katika tukio hilo akiwa amevaa gauni jeupe lililovutia wengi.

Beyonce amerudi Met Gala 2026 kama mmoja wa waratibu (co-chair) baada ya kutokuwepo kwa takribani muongo mmoja. Ingawa hajawahi kuwa na mgogoro wa moja kwa moja na waandaaji wa Met Gala, kutokuwepo kwake kwa muda mrefu kumehusishwa na uvumi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na masuala ya kibinafsi.

Kwa upande mwingine, Blake Lively aliwashangaza mashabiki kwa kurejea kwenye zulia jekundu muda mfupi baada ya kumaliza mgogoro wa kisheria na Justin Baldoni uliokuwa ukihusishwa na filamu It Ends With Us. Muonekano wake wa gauni la rangi ya pastel uliashiria utulivu mpya baada ya changamoto hizo.

Mastaa wengine waliojitokeza ni pamoja na Nicole Kidman, aliyeng’aa kwa mavazi ya Chanel, pamoja na Bad Bunny aliyebadili kabisa muonekano wake kwa mapambo ya uso.

Beyonce akiwa na mtoto wake Blue Ivy

Aidha, Kim Kardashian na mama yake Kris Jenner walionyesha mvuto wa kipekee, huku Tyla akivutia kwa vazi la ujasiri.

Wengine waliohudhuria ni Ashley Graham, Charli XCX, Claire Foy na Zoë Kravitz.

Kwa upande wake, Katy Perry alivutia kwa mavazi yenye mandhari ya anga, akionekana kuvaa kofia ya mwanaanga.

Kim Kardashian akiwa na mama yake Kris Jenner.
Mwigizaji, mwimbaji na mwanamitindo kutoka Marekani, Zoe Kravitz
Nyota wa zamani wa mchezo wa tenesi Mmarekani, Venus Williams.
Msanii maarufu wa muziki kutoka Uingereza, Charli Xcx
Mwigizaji, mwimbaji na mwanamitindo Kendall Jenner

Mwanamitindo na Mtangazaji, Heidi Klum.

Leave a Comment