×

Jasinta Makwabe Aeleza Kisa Cha Kushtua Cha Mwanaume Aliyemdanganya Akafanya Send-off

Msanii na mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Jasinta Makwabe.

Msanii na mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Jasinta Makwabe, akiwa katika mahojiano na kituo kimoja cha redio amesema anatamani sana kuolewa na kuwa na familia yake, akifichua kuwa aliwahi kusali kwa muda mrefu akiomba apate mume bora wa maisha yake na apate watoto ndani ya ndoa.

Hata hivyo, alieleza kuwa katika harakati hizo aliwahi kukutana na changamoto kubwa baada ya mwanaume mmoja aliyekuwanaye kwenye mahusiano kukodi watu waliodaiwa kuwa wazazi wake ili kumshawishi kuwa anampenda kwa dhati, hali iliyosababisha kuanza mipango ya ndoa hadi kufikia hatua ya kufanya send-off siku ya Valentine Day mwaka jana.

Baada ya kufanya send-off ndipo alipogundua kuwa mwanaume huyo alikuwa tayari ameshafunga ndoa na alikuwa na watoto, jambo lililosababisha harusi kutokufanyika, licha ya awali kudanganywa kuwa ameachana na mke wake.

Aidha, Jasinta amemuelezea mwanaume huyo kuwa si Mtanzania na hakuwa maarufu sana, na alikuwa akiishi nje ya nchi. Alisema kuwa ilipofika siku ya harusi, mambo yalibadilika na akagundua ukweli wote, jambo lililomfanya aachane na mpango huo.

Pia amekiri kuwa alikurupuka kuingia kwenye mahusiano hayo kwa lengo la kuolewa bila kumfahamu vizuri mwanaume huyo, jambo ambalo limempa somo kubwa maishani. Ameongeza kuwa sasa hataki kulipiwa kodi na mwanaume yeyote, na anajitegemea kifedha, akithibitisha kuwa amenunua gari kwa pesa yake na anaishi maisha yake huru, wakati mwingine akitumia usafiri wa bodaboda.

Credit; WasafiFM

Leave a Comment