×

Mwenyekiti wa Kikundi cha Sera cha GSMA Afrika Ataka Mageuzi ya Kikodi

Mkuu wa Udhibiti wa Airtel Africa na Mwenyekiti wa Kundi la Sera Afrika la GSMA, Daddy Mukadi

KINSHASA, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mei 5, 2026 – Mkuu wa Udhibiti wa Airtel Africa na Mwenyekiti wa Kundi la Sera Afrika la GSMA, Bw. Daddy Mukadi, ametoa wito kwa serikali za Afrika kutambua sekta ya mawasiliano ya simu kama nguzo kuu ya uchumi na kutekeleza mageuzi mawili mahususi ya kodi yanayoweza kuharakisha kwa kiasi kikubwa ujumuishaji wa kidijitali barani.

Akizungumza katika toleo la kwanza la mkutano wa États Généraux du Secteur des Postes et Télécommunications uliofanyika Kinshasa, DRC—hafla iliyolenga kuandaa dira ya kimkakati ya sekta ya kidijitali na mawasiliano nchini humo na kuhudhuriwa na Rais Félix Tshisekedi Bw. Mukadi, ambaye pia ni mwanachama wa Kundi la Sera la Kimataifa la GSMA, aliwataka wadau wa serikali na sekta binafsi kufikiria upya nafasi ya mawasiliano ya simu katika maendeleo ya kitaifa.

Alisisitiza kuwa sekta hiyo haipaswi tena kuonekana kama sekta saidizi pekee, bali kama mhimili mkuu wa maendeleo ya uchumi wa bara.
“Sekta ya mawasiliano haiwezi tena kuchukuliwa kama ya kusaidia tu. Sasa ni sekta ya msingi. Sekta zote kuanzia usalama, fedha, usafiri hadi afya zinategemea teknolojia ya kidijitali kwa ukuaji,” alisema.

Kauli zake zinakuja katika wakati muhimu kwa uchumi wa kidijitali barani Afrika. Kwa mujibu wa ripoti ya Mobile Economy Africa 2025 ya GSMA, sekta ya simu ilichangia dola za Marekani bilioni 220 katika uchumi wa Afrika mwaka 2024, sawa na asilimia 7.7 ya Pato la Taifa (GDP), na inatarajiwa kufikia dola bilioni 270 ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo, licha ya mitandao ya simu kufikia asilimia 95 ya watu barani Afrika, takribani asilimia 75 ya wananchi bado hawajaunganishwa na huduma za intaneti—changamoto inayochangiwa zaidi na gharama kubwa za vifaa vya kidijitali.

Kutokana na hali hiyo, Bw. Mukadi alipendekeza maboresho ya sera za umma pamoja na mifumo ya kisheria na udhibiti ili kupanua upatikanaji wa huduma za kidijitali. Alisisitiza kuwa sekta ya mawasiliano inapaswa kutambuliwa kama nguzo ya msingi ya maendeleo ya uchumi, huku wadau wakishirikiana kuongeza uwekezaji, kupanua wigo wa huduma na kupunguza pengo la matumizi ya huduma hizo.

Aidha, alitaja vikwazo vikuu vinavyozuia ujumuishaji wa kidijitali kuwa ni pamoja na gharama za simu janja na ushuru wa uagizaji wa miundombinu ya mawasiliano. Alipendekeza kusamehe ushuru na kodi kwa muda wa miaka miwili hadi mitatu kwa simu janja za bei nafuu (kati ya dola 40 hadi 150) ili kusaidia kupunguza pengo la matumizi.

Pia alipendekeza kuondolewa kwa ushuru wa kuingiza vifaa vya mawasiliano kwa angalau miaka mitatu ili kuchochea upanuzi wa mtandao.

Aliongeza kuwa, hatua hizi “zitasaidia kuleta teknolojia jumuishi na endelevu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii,” akiongeza kuwa zitachochea kasi ya muunganiko, kuboresha upatikanaji wa huduma na kuwezesha watu, biashara na jamii nyingi zaidi kushiriki katika uchumi wa kidijitali.

Alissisitiza kuwa ni muhimu kwa serikali na sekta binafsi kushirikiana kwa karibu kuunda mazingira ya udhibiti yanayochochea ubunifu, kulinda watumiaji na kuhimiza uwekezaji wa muda mrefu.

OBAMA – “SIYO RAHISI KUISHINDA IRAN – NETANYAHU ALINISHAWISHI KUISHAMBULIA NIKAGOMA TRUMP KAKUBALI”

Leave a Comment