
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Mei 6, 2026, Petroli imeongezeka kutoka Tsh. 3,820 hadi 4,115 kwa Lita, huku Dizeli kutoka Tsh. 3,806 hadi 4,248 kwa Dar es Salaam.
EWURA imeeleza mabadiliko ya bei hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na vita inayoendelea eneo la Mashariki ya Kati, ikihusisha Marekani, Israel na Iran, pamoja na kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz unaopitisha takriban 20% ya mafuta yote yanayosafirishwa Duniani kumeathiri upatikanaji na gharama za mafuta katika soko la kimataifa.
Baadhi ya mikoa ambayo bei ya Petroli ipo juu zaidi ni Mwanza, Kigoma, Geita, Kagera na Katavi. ambapo ni zaidi ya Tsh. 4,300.
