×

Mchumba wa Ashlee Jenae Avunja Ukimya kwa Mara ya Kwanza, Atoa Pole Kwa Familia

Mshawishi maarufu wa mitandaoni mtandaoni Ashly Robinson, maarufu kama Ashlee Jenae, aliyefariki ghafla akiwa safarini nchini Tanzania, tukio lililoacha maswali mengi na majonzi makubwa kwa familia na mashabiki wake.

Mchumba wake, Joe McCann, amevunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu kifo hicho kilipotokea. Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Joe alieleza huzuni yake kubwa akisema hana maneno ya kuelezea maumivu, pengo na mshtuko alioupata baada ya kumpoteza mpenzi wake.

Joe pia alitoa pole kwa wazazi wa marehemu, Yolanda Endres na Harry Robinson, akieleza kuwa kifo hicho ni janga lisiloelezeka. Aliongeza kuwa Ashlee alikuwa na ndoto kubwa ya kuwa mama na kuanzisha familia, na anaamini angekuwa mama bora sana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, Ashlee alipatikana akiwa hana fahamu ndani ya villa waliyokuwa wamefikia, kabla ya kukimbizwa hospitali ambako alithibitishwa kufariki. Safari hiyo ilikuwa ya mapumziko, siku chache tu baada ya Joe kumpa pete ya uchumba.

Awali, vyombo vya usalama vilikuwa vinaelekea kuhusisha kifo hicho na uwezekano wa kujiua, lakini familia ya marehemu imepinga vikali madai hayo na sasa inafanya uchunguzi wake binafsi ili kubaini chanzo halisi cha kifo.

Ingawa mwili wa Ashlee tayari umerejeshwa kwa familia yake, bado kuna maswali kuhusu mali zake binafsi, ikiwemo pete ya uchumba ambayo haijarejeshwa hadi sasa.

Uchunguzi unaendelea, huku wengi wakisubiri majibu yatakayotoa ukweli juu ya kilichosababisha kifo cha ghafla cha nyota huyo wa mitandao.

KUPOTEA kwa MABINTI WAWILI ARUSHA – ALIYETAJWA KUWA MPENZI AKAMATWA BAADA ya KURIPOTI POLISI..

Leave a Comment