×

Polisi Wakamata Watuhumiwa 4 Mauaji ya Mwanafunzi wa IFM Aliyekatwa Kichwa – Video

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya kikatili ya mwanafunzi wa Chuo cha IFM, James Rogers Temba, ambaye mwili wake ulikutwa ukiwa hauna kichwa katika mto Msimbazi, eneo la Kipawa, Ilala.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Polisi, mwili wa marehemu ulionekana ukielea majini mnamo Aprili 30, 2026, jambo lililozua taharuki miongoni mwa wananchi na kuanzisha uchunguzi wa kina.

Katika hatua ya awali ya uchunguzi, Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wanaohusishwa na tukio hilo. Watuhumiwa hao ni pamoja na Steven Rogers Chaka (31), Anna Frank Lema (30), Twalibu Khamis (23), na Michael John (26), wote wakiwa na makazi katika maeneo tofauti nchini.

Jeshi la Polisi limesema linaendelea kukusanya ushahidi zaidi, ikiwemo uchambuzi wa vielelezo muhimu vinavyoweza kusaidia kufanikisha uchunguzi huo na kufikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.

Aidha, wananchi wametakiwa kuwa watulivu huku wakishauriwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kukamilisha uchunguzi huo.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Leave a Comment