
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuwahoji watu mbalimbali kuhusiana na tukio la kupotea kwa wasichana wawili ambao ni Rahma Nakivoka Toroka (22) na Karen Mark Didas (23) wote wakazi wa Arusha.
Taarifa ya leo Mei 06, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha imeeleza kuwa pamoja na taarifa mbalimbali ambazo zimeshakusanywa, Jeshi hilo limetoa wito kwa yoyote mwenye taarifa ambazo zinaweza kusaidia kufanikisha uchunguzi huu, asisite kuzifikisha kwani zitapokelewa na kufanyiwa kazi kwa haraka.
