Rais Samia Ahitimisha Mafunzo ya Uongozi TCT Ukonga (Picha +Video)
Global Publishers May 9, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa kwenye uwanja wa Gwaride katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, alihudhuria hafla maalum iliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam, tarehe 09 Mei 2026.
Katika hafla hiyo, Rais Samia alihitimisha rasmi Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi Namba 28 pamoja na Uongozi Daraja la Pili Kozi Namba 48 kwa mwaka wa mafunzo 2025/2026. Tukio hilo lilihusisha gwaride la heshima lililoonesha nidhamu, ukakamavu na maandalizi ya viongozi wanaoandaliwa kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kwa Wahitimu waliofanya vizuri kwenye Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 kwa Mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.