
Klabu ya USM Alger imepiga hatua muhimu kuelekea ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Zamalek SC katika mchezo wa kwanza wa fainali uliopigwa nchini Algeria.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 90+8 kupitia kwa Ahmed Khaldi na kuipa USM Alger ushindi muhimu wa nyumbani kabla ya mchezo wa marudiano.
Katika dakika za mwisho za mchezo huo, Mahmoud Bentayg alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 90+6, jambo lililoiongezea presha Zamalek kuelekea mchezo wa pili.

Mchezo wa marudiano wa fainali hiyo unatarajiwa kupigwa Mei 16, 2026 ambapo bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2025/26 atapatikana.
FT: USM Alger 1-0 Zamalek SC
⚽ 90+8’ Ahmed Khaldi
🟥 90+6’ Mahmoud Bentayg
Ikumbukwe kuwa USM Alger ilitwaa ubingwa wa CAF Confederation Cup msimu wa 2022/23 kwa faida ya bao la ugenini dhidi ya Young Africans SC baada ya sare ya jumla ya mabao 2-2.