
Katika tukio lililovuta hisia za mashabiki wengi, Cardi B na Stefon Diggs wameonekana pamoja tena katika hafla ya Siku ya Akina Mama iliyofanyika Washington, D.C., iliyoandaliwa na Diggs Deep Foundation.
Katika picha na video zilizosambaa mtandaoni, wawili hao walionekana wakiwa na tabasamu kubwa, wakikumbatiana na kucheka huku wakipiga picha mbele ya mandhari ya waridi iliyopambwa kwa ajili ya hafla hiyo. Stefon Diggs pia alionekana akimbusu Cardi B shavuni, akiwa amemshika kiunoni kwa upole, jambo lililoamsha mijadala mikubwa mitandaoni.
Wapenzi wa mastaa hao walishangazwa na uhusiano wao wa karibu, hasa kutokana na taarifa zilizokuwa zimesambaa awali zikidai kwamba wawili hao walikuwa wametengana mapema mwaka huu. Hali hii imefanya baadhi ya mashabiki kuamini kwamba huenda wamefufua tena uhusiano wao, ingawa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa pande zote mbili.
Hadi sasa, Cardi B na Stefon Diggs hawajatoa kauli yoyote kuhusu hali ya uhusiano wao, na hivyo kuacha nafasi kubwa ya uvumi kuendelea kusambaa mtandaoni.
Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona kama tukio hilo ni ishara ya upendo uliorejea au ni urafiki wa kawaida uliotokana na hafla ya kijamii.