
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 12 Mei 2026 amewasili katika Entebbe International Airport nchini Uganda kwa ajili ya kushiriki Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni.
Mara baada ya kuwasili katika uwanja huo wa ndege, Rais Dkt. Samia alipokelewa na kusalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Tatu wa Uganda, Rukia Isaya Nakadama, pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya Uganda.
Sherehe za uapisho wa Rais Museveni zinatarajiwa kufanyika katika Kololo Ceremonial Grounds jijini Kampala, ambapo viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika na duniani wanatarajiwa kuhudhuria.
Ushiriki wa Rais Dkt. Samia katika hafla hiyo unaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda.

