
Mwandishi wetu
Mchekeshaji mwenye title kubwa Bongo, MC Pilipili anatarajiwa kuwavunja watu mbavu katika Tour ya Nasikia Harufu ya Samaki ambayo ameamua kuanza kuifanya Kanda ya Ziwa kuanzia Ijumaa Kuu.
Katika tour hiyo, MC Pilipili ataanza mambo mkoani Geita ambapo viingilio vitakuwa shilingi 15,000 kwa VIP na kawaida 10, 000.
Baada ya hapo, atawavunja mbavu watu katika mkesha wa Pasaka ndani ya Klabu ya Masai huko Kahama mkoani Shinyanga kwa kiingilio cha shilingi 7,000.
Baada ya hapo, tour hiyo itamalizwa katika Siku ya Pasaka ambapo watu watavunjwa mbavu katika Ukumbi wa Gold Crest, jijini Mwanza ambapo viingilio vitakuwa shilingi 30,000 kwa VIP na 10,000 kawaida.
Ili kuhakikisha kunakuwa na burudani ya kufa mtu, MC Pilipili atakuwa na wachekeshaji wengine kama Dogo Pepe, Oscar Nyerere na Katarina Karatu. Mbali na uchekeshaji, mwanamuziki anayefanya vizuri, Barnabas atakuwepo kutoa burudani ya nguvu.