×

Zari Athibitisha Kuvunjika kwa Ndoa Yake na Shakib Cham Baada ya Miaka Mitano

Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu, Zari Hassan, ametangaza rasmi kuachana na mume wake, Shakib Cham, baada ya kuwa pamoja kwa takribani miaka mitano.

Zari amethibitisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo amesema yeye na Shakib wamefikia uamuzi wa kutengana baada ya kushindwa kutatua tofauti zilizokuwepo katika mahusiano yao licha ya juhudi mbalimbali za kuyarekebisha.

Katika ujumbe wake, Zari amesema uamuzi huo haukuwa rahisi kuufikia, lakini baada ya kutafakari kwa kina kuhusu mustakabali wao, wameona ni hatua sahihi kwa pande zote mbili.

Aidha, amesisitiza kuwa kuachana kwao hakujatokana na chuki wala migogoro mikubwa, bali ni uamuzi walioufanya kwa maelewano na heshima. Ameeleza kuwa wataendelea kuheshimiana na kubaki marafiki hata baada ya kutengana.

Zari pia alimshukuru Shakib kwa kipindi walichokaa pamoja, akieleza kuwa wanabaki na kumbukumbu nyingi nzuri walizozijenga pamoja pamoja na sapoti waliyopeana katika maisha yao.

Tangazo hilo limezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku mashabiki na wafuasi wao wakituma ujumbe wa kuwapa moyo wawili hao katika kipindi hiki cha mabadiliko ya maisha yao.

Leave a Comment