
Ubora wa rasilima watu( Afya na Maarifa) ndio sarafu ya dunia kwa sasa na hivyo kete muhimu kwa Tanzania kujiunga na Mataifa tajiri mwaka 2050( Trilioni dola Club).
Wauguzi ndio Nguzo ya Rasilimali Watu na Mhimili wa Uchumi wa Dola Trilioni 1 (2050)
Katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, tunatambua kuwa uuguzi si kazi tu, bali ni wito wa kitume unaohitaji upendo, subira, na utu wa hali ya juu. Wauguzi ni daraja kati ya wagonjwa na kupona, wakiwa mstari wa mbele kuokoa maisha.
Bila afya bora, hakuna tija kazini; wauguzi wanahakikisha jamii ina afya, na hivyo kuwa kiungo muhimu kimkakati katika kujenga uchumi mkubwa.
Tanzania inalenga kujiunga na “Club” ya nchi zenye uchumi wa kuanzia dola trilioni moja ifikapo 2050. Hata hivyo, ili kufika huko, tunahitaji rasilimali watu yenye afya bora.
Pamoja na uwekezaji mkubwa wa kibajeti kuboresha miundomibinu ya huduma, vifaa tiba, dawa, wauguzi na madaktari uliofanywa na Serikali, Bado kuna changamoto kubwa ya uwiano idadi ya wauguzi kwa idadi ya watu.Wakati WHO inapendekeza uwiano wauguzi kwa idadi ya watu kuwa wauguzi 45 kwa watu 10,000, Afrika kwa wastani bado ipo chini sana ikiwa na wastani wa wauguzi 18 kwa watu 10,000. Huku nchi tajiri duniani, zimefika uwiano wa wauguzi100 kwa watu 10,000.
Hii inamaanisha uwekezaji wetu katika uuguzi lazima uongezeke mara dufu kuelekea kujiunga na nchi hizo kama tulivyokubaliana kwenye Dira2050, Na kufikia hilo
hatuwezi kutegemea serikali pekee.
Mchango wa sekta binafsi ni muhimu sana:Takwimu zinaonesha Sekta binafsi nchini Tanzania inatarajiwa kuchangia asilimia 70 (Tsh Trilioni 334) ya gharama za Mpango wa Maendeleo wa Taifa ifikapo 2026/27- 2030/31.
Zaidi ya asilimia 50 ya matumizi ya afya yanachangiwa na sekta binafsi, na takriban 40% ya vituo vya afya vinamilikiwa au kuendeshwa na sekta binafsi nchini.
Changamoto ya sekta hii ni mtambukwa, Na ina wajibu wa pande zote. Kwa upande wa Serikali ni kuendelea kuimarisha Ubia kati yake na Sekta Binafsi na dhana nzima ya uwekezaji kama inavyosisitizwa na Rais wetu Dr SSH, lakin kwa upande wa wananchi ni kutekeleza uzazi wa Mpango kwani kuna uhusiano mkubwa kati ya umasikini na kasi ya ongezeko la watu hasa katika nchi masikini ambazo uwezo wa serikali kutoa afya na elimu bora kwa kaya masikini bado changamoto kubwa.
Nikatika juhudi za kuongeza uwezo wa kugharimia sekta muhimu kama Afya na Elimu kwa masikini, tunaendelea kusisitiza PPP ili Serikali iendelee kuachana na kuwekeza maeneo yenye mvuto wa sekta binafsi na inachokiokoa kisaidie maeneo kama afya kwa masikini ambayo hayana mvuto kwa Sekta Binafsi kwakuwa hayalipi kibiashara lakin ni muhimu kwa uchumi na ustawi wa Taifa.
Wauguzi ndio uhai wa sekta ya afya. Uwekezaji katika wauguzi ni uwekezaji katika uchumi wetu.
Kazi ya kipekee ya muuguzi ni kumsaidia mtu, mgonjwa au mzima, katika kufanya shughuli zile zinazochangia afya au kupona (au kifo cha amani), ambazo angeweza kufanya bila kusaidiwa kama angekuwa na nguvu, utashi, au maarifa ya kutosha. Heri ya Siku ya Wauguzi. Changamoto ni nyingi lakini lipo tumaini kadiri tunavyojenga na kufungua uchumi! Upo uhusiano mkubwa kati ya ukubwa wa uchumi na ubora wa maisha ya wauguzi