
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Allan Okello amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu ya soka ya NBC msimu wa mwaka 2025/26 baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo mitatu aliyocheza mwezi huo, akifunga bao moja na kuhusika na mengine sita kwa dakika 320 alizocheza.
Okello alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Pacome Zouzoua wa Yanga na Idd Selemani wa Azam FC, alioingia nao fainali katika mchakato wa tuzo za mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
