×

Kichwa cha Marehemu James Temba Chapatikana Kitunda Kibeberu Ilala, Dar – Video

Marehemu James Temba enzi za uhai wake.

Kichwa cha marehemu James Temba ambaye alifariki kwa mazingira ya kutatanisha na kukuza simanzi kwa familia na jamii, kimepatikana siku chache baada ya mazishi yake kufanyika.

Akizungumza na Global TV, Baba wa marehemu Mzee Temba amesema kuwa taarifa za awali walizopokea kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa kichwa hicho kimepatikana katika eneo la Kitunda Kibeberu, Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Marehemu James Temba alipoteza maisha kwa mauaji ya kikatili yaliyozua masikitiko makubwa kwa ndugu, jamaa na wananchi.

Hadi sasa Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini waliohusika pamoja na chanzo cha mauaji hayoiyotikisa jamii.

Leave a Comment