Mapokezi Aliyoyapata Rais wa Marekani Trump Yaweka Hostoria Beijing – Picha
Global Publishers May 15, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa China Xi Jinping akinyanyua glasi ya mvinyo maalum wakati alipomkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika chakula cha kitaifa kilichoandaliwa kwenye ukumbi wa Great Hall of the People, Mei 14, 2026 jijini Beijing, China.
Rais wa Marekani Donald Trump amepokelewa kwa heshima kubwa nchini China baada ya kuwasili jijini Beijing katika ziara inayotajwa kuwa muhimu kwa mahusiano ya kiuchumi na kisiasa kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani.
Trump aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Beijing Capital akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Marekani pamoja na wakurugenzi wakubwa wa kampuni za kimataifa, huku China ikiandaa mapokezi ya zulia jekundu na ulinzi mkali wa heshima.
Rais wa Marekani Donald Trump akinywa mvinyo wakati wa chakula cha kitaifa kilichoandaliwa na Rais wa China Xi Jinping katika ukumbi wa Great Hall of the People, Mei 14, 2026 jijini Beijing, China.
Miongoni mwa waliokuwa katika msafara huo ni Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth, bilionea Elon Musk pamoja na mwanzilishi na CEO wa Nvidia Jensen Huang. Pia watoto wa Trump, Eric Trump na Lara Trump, walionekana kushuka kutoka ndege ya Air Force One wakati wa mapokezi hayo.
Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo ya ana kwa ana na Trump kuhusu biashara, uwekezaji, teknolojia ya akili bandia (AI) pamoja na mvutano wa ushuru wa bidhaa kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Marekani Donald Trump akinywa mvinyo.
Ziara hiyo imevutia pia viongozi wa kampuni kubwa za Marekani kama Apple, Tesla, Boeing na BlackRock ambao wanatafuta kuongeza ushirikiano wa biashara ndani ya soko kubwa la China.
China imeonyesha nia ya kufungua zaidi milango kwa kampuni za Marekani huku ikisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kiuchumi badala ya migogoro ya kibiashara ambayo imekuwa ikiathiri uchumi wa dunia katika miaka ya hivi karibuni.
Rais wa China Xi Jinping (wa pili kushoto) na Rais wa Marekani Donald Trump (katikati) wakipeana mikono.Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla, Elon Musk, alihudhuria chakula cha kitaifa kilichoandaliwa na Rais wa China Xi Jinping.Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akiwa katika ukumbi wa Great Hall of the People jijini Beijing.Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na Rais wa Marekani Donald Trump wakitembelea Hekalu la Mbinguni (Temple of Heaven) jijini Beijing Mei 14, 2026.
Rais wa Marekani Donald Trump akisindikizwa na Makamu wa Rais wa China Han Zheng (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Beijing Capital jijini Beijing, Mei 13, 2026.
Askari wa heshima wa Jeshi la Ukombozi wa Wananchi wa China (PLA) wakisimama na bendera za Marekani na China mbele ya ukumbi wa Great Hall of the People kabla ya hafla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Marekani Donald Trump jijini Beijing, Mei 14, 2026.
Rais wa China Xi Jinping (kulia) na Rais wa Marekani Donald Trump (katikati) wakitembelea Hekalu la Mbinguni (Temple of Heaven) jijini Beijing Mei 14, 2026.Rais wa Marekani Donald Trump akiwa mbele akifuatwa na Rais wa China Xi Jinping, akisalimiana na maafisa mbalimbali katika ukumbi wa Great Hall of the People jijini Beijing, Mei 14, 2026.
Rais wa Marekani Donald Trump alivyowasili kwa ndege ya Air Force One katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital wakati wa ziara yake nchini China, Mei 13, 2026.