×

China Yampa Rais wa Marekani Donald Trump Mapokezi ya Kifalme Beijing – Picha

Rais wa Marekani Donald Trump amepokelewa kwa heshima kubwa nchini China baada ya kuwasili jijini Beijing katika ziara inayotajwa kuwa muhimu kwa mahusiano ya kiuchumi na kisiasa kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani.

Trump aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Beijing Capital akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Marekani pamoja na wakurugenzi wakubwa wa kampuni za kimataifa, huku China ikiandaa mapokezi ya zulia jekundu na ulinzi mkali wa heshima.

Miongoni mwa waliokuwa katika msafara huo ni Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth, bilionea Elon Musk pamoja na mwanzilishi na CEO wa Nvidia Jensen Huang. Pia watoto wa Trump, Eric Trump na Lara Trump, walionekana kushuka kutoka ndege ya Air Force One wakati wa mapokezi hayo.

Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo ya ana kwa ana na Trump kuhusu biashara, uwekezaji, teknolojia ya akili bandia (AI) pamoja na mvutano wa ushuru wa bidhaa kati ya nchi hizo mbili.

Ziara hiyo imevutia pia viongozi wa kampuni kubwa za Marekani kama Apple, Tesla, Boeing na BlackRock ambao wanatafuta kuongeza ushirikiano wa biashara ndani ya soko kubwa la China.

China imeonyesha nia ya kufungua zaidi milango kwa kampuni za Marekani huku ikisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kiuchumi badala ya migogoro ya kibiashara ambayo imekuwa ikiathiri uchumi wa dunia katika miaka ya hivi karibuni.

 

Leave a Comment