
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Mei 16, 2026 amekutana na Mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria na Mwanzilishi wa Dangote Group, Aliko Dangote, katika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji kati ya Tanzania na sekta binafsi ya Afrika, hususan katika maeneo ya viwanda, biashara na maendeleo ya miundombinu.

Dangote ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa barani Afrika kupitia kampuni yake ya Dangote Group inayojihusisha na uzalishaji wa saruji, sukari, mbolea pamoja na sekta nyingine muhimu za uchumi.
Kwa upande wake, Serikali ya Tanzania imeendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kupitia maboresho mbalimbali ya mazingira ya biashara yanayolenga kukuza uchumi na ajira kwa wananchi.


