×

WHO Yatoa Tahadhari Kufuatia Mlipuko Mpya wa Ebola Afrika

Shirika la Afya Duniani,  limetangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuwa dharura ya afya ya kimataifa kufuatia ongezeko la visa na hofu ya kusambaa katika mataifa jirani.

Kwa mujibu wa WHO, mlipuko huo umeathiri zaidi eneo la Ituri Province ambapo takribani visa 246 vinashukiwa kuripotiwa huku zaidi ya watu 80 wakifariki dunia.

Shirika hilo limesema aina ya Ebola iliyobainika ni virusi vya Bundibugyo ambavyo hadi sasa havina chanjo wala dawa rasmi iliyothibitishwa kutibu ugonjwa huo.

Maambukizi tayari yamethibitishwa katika miji ya Bunia, Kinshasa na Goma huku visa viwili pia vikithibitishwa nchini Uganda.

WHO imeeleza kuwa hali ya usalama mashariki mwa DR Congo, migogoro ya mara kwa mara, pamoja na wananchi kusafiri kwa wingi kati ya mipaka vinaongeza hatari ya maambukizi kuenea zaidi ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali, maumivu ya misuli, uchovu mkubwa, kuumwa kichwa, kutapika, kuharisha na katika hatua kali mgonjwa anaweza kuvuja damu.

Kutokana na hali hiyo, WHO imezitaka nchi jirani kuongeza uangalizi mipakani, kufuatilia wagonjwa mapema na kuweka mifumo madhubuti ya kudhibiti maambukizi ili kuzuia mlipuko huo kuwa mkubwa zaidi.

MELI KUBWA YA KIVITA YA MAREKANI USS GERALD R. FORD YATUA -VIRGINIA-OPERESEHENI YA MASHARIKI YA KATI

Leave a Comment