×

Trump Aionya Iran Tena, Asema “Hakutakuwa na Chochote Kitakachosalia”

Rais wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameionya Iran kuwa muda wa kufikia makubaliano ya kumaliza vita unaendelea kuyoyoma huku mazungumzo kati ya pande hizo yakiripotiwa kukwama.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye jukwaa lake la Truth Social, Trump amesema Iran inapaswa kuchukua hatua haraka kabla hali haijawa mbaya zaidi.

“Ni bora waanze kuchukua hatua haraka, la sivyo hakutakuwa na chochote kitakachosalia kwao,” aliandika Trump.

Kauli hiyo imekuja wakati Rais huyo wa Marekani akitarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuhusu hali ya mzozo huo unaoendelea Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa Marekani haijatoa majibu yenye mwafaka kuhusu mapendekezo ya hivi karibuni yaliyowasilishwa na Tehran kwa ajili ya kumaliza vita.

Shirika la habari la Mehr limedai kuwa ukosefu wa maridhiano kutoka Marekani kunaweza kusababisha mazungumzo hayo kusimama kabisa.

Trump pia aliwahi kueleza mapema wiki hii kuwa mazungumzo ya kusitisha mapigano yako katika hatua mbaya sana kuendelea kuwepo baada ya Marekani kuyakataa baadhi ya masharti yaliyowekwa na Iran, akisema hayakubaliki kabisa.

Mvutano huo unaendelea kuzua hofu ya kuongezeka kwa hali ya sintofahamu katika eneo la Mashariki ya Kati huku mataifa mbalimbali yakifuatilia kwa karibu hatma ya mazungumzo hayo.

CHRISTINA wa TRA AKUBALI MZIKI wa SIMBA – AFUTA KAULI YAKE ya WANAUME wa DAR -“NAENDA KUSHITAKI”

Leave a Comment