
Nairobi, Kenya — Mwanamke aliyefahamika kama Rachel Wandetto aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Kenyatta National Hospital amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika tukio linalodhaniwa kuwa shambulio la petroli eneo la Mwiki, Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen, marehemu alifariki leo asubuhi ya Jumatatu Mei 18, 2026 akiwa hospitalini, ambapo alikuwa akiendelea kupatiwa huduma za kitabibu kufuatia majeraha aliyoyapata katika tukio hilo.
Murkomen amesema amesikitishwa na kifo hicho, akikitaja kama tukio la kusikitisha na kulaani vikali kitendo hicho alichokiita cha kinyama kilichofanywa na kundi la watu wasio na uvumilivu.
Vyombo vya usalama nchini Kenya vinaendelea na uchunguzi kubaini mazingira halisi ya tukio hilo pamoja na waliohusika, huku mamlaka zikiahidi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika.