
Yanga wamefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex.
Nyota wa mchezo huo alikuwa Allan Okello, ambaye alifunga mabao mawili na kufikisha jumla ya magoli 9 kwenye ligi msimu huu.
- 14’ — Okello (Yanga SC)
- 42’ — Mudathir Yahya
- 69’ — Okello
Kiungo Mudathir Yahya aliongeza bao la pili kabla ya mapumziko, huku Okello akihitimisha ushindi huo katika kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo, Yanga Ssasa wanaongoza ligi wakiwa na alama 57 baada ya mechi 24, wakizidi kwa alama mbili Simba ambao walikuwa wamekaa kileleni kwa chini ya saa 24 kabla ya kupitwa tena.
Ushindi huu unaendelea kuongeza ushindani mkali wa ubingwa kati ya vigogo hao wawili wa soka la Tanzania, huku msimu ukiendelea kuelekea hatua za mwisho.