
Mbunge wa Jimbo la Buchosa mkoani Mwanza, Eric Shigongo, ametaka kutungwa sheria maalumu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuwasaidia Watanzania kushindana na wawekezaji wanaotoka nje ya nchi.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Mei 22, 2026 bungeni jijini Dodoma, Shigongo amesema Tanzania inahitaji kuwawezesha wazawa kupitia mitaji nafuu, mikopo yenye riba ndogo pamoja na sera zinazowalinda kwenye ushindani wa biashara.
“Wageni tunawapenda lakini Mtanzania awezeshwe kushikilia uchumi wa nchi yake, hakuna nchi isiyolinda watu wake kwenye uchumi, amesema Shigongo.
Pia, Shigongo ameishauri Serikali kuendelea kuvutia wawekezaji wa nje huku ikiweka mazingira bora yatakayowasaidia Watanzania kunufaika zaidi na rasilimali pamoja na fursa za kiuchumi zilizopo nchini.