×

Mamelodi Sundowns Watwaa Ubingwa wa Pli wa Ligi Ya Mabingwa, Yaichapa AS FAR

Mamelodi Sundowns wametwaa ubingwa wa pili wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa baada ya kuichapa AS FAR kwa jumla ya mabao 2-1 katika fainali ya msimu wa 2025/26.

Miamba hiyo ya Afrika Kusini iliingia mchezo wa marudiano ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 walioupata nyumbani, kabla ya kutoka sare ya 1-1 ugenini kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat, Morocco.

Katika mchezo huo, AS FAR walitangulia kupata bao kupitia Hrimat dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti, lakini Teboho Mokoena aliisawazishia Sundowns dakika ya 45+7 na kuzima ndoto za wenyeji hao.

Matokeo hayo yaliwafanya Mamelodi Sundowns kutwaa taji lao la pili la CAF Champions League na kuendelea kuandika historia mpya katika soka la Afrika.

Leave a Comment