×

Nafasi 30 za Huduma kwa Wateja Zatangazwa na Vunjabei Bet, Mwisho wa Maombi Mei 30

Kampuni ya michezo ya kubashiri mtandaoni VUNJABet imetangaza nafasi 30 za ajira kwa ajili ya wahudumu wa huduma kwa wateja (Customer Care) ikiwa ni sehemu ya kupanua huduma zake kwa wateja nchini.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kampuni hiyo inatafuta vijana wenye uwezo mzuri wa mawasiliano, nidhamu ya kazi pamoja na uelewa wa matumizi ya mifumo ya kidigitali ili kujiunga na timu yake inayohudumia wateja kwa njia mbalimbali za mawasiliano.

Waombaji wanatakiwa kuwa na elimu ya angalau kidato cha sita au zaidi, uwezo wa kutumia kompyuta pamoja na uzoefu katika huduma kwa wateja ukiwa ni sifa ya ziada.

VUNJABet imeeleza kuwa nafasi hizo zinatoa fursa kwa vijana wengi kujifunza na kufanya kazi katika sekta ya michezo ya kubashiri ambayo inaendelea kukua kwa kasi nchini Tanzania.

Kampuni hiyo imewataka wenye sifa kuwasilisha maombi yao mapema kupitia njia zilizotajwa kwenye tangazo rasmi la ajira.

Leave a Comment