×

Rais Museveni Amteua Mke Wake Kuwa Waziri wa Elimu na Michezo

Mke wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Janet Museveni

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemteua tena mkewe, Janet Museveni kuendelea kuhudumu kama Waziri wa Elimu na Michezo katika Baraza jipya la Mawaziri la muhula wa 2026–2031.

Janet Museveni ameendelea kushikilia wizara hiyo tangu mwaka 2016 alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kuiongoza sekta ya elimu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda. Kabla ya hapo aliwahi kuwa Waziri wa Masuala ya Karamoja kuanzia mwaka 2009 hadi 2011 na baadaye Waziri wa Maendeleo ya Jamii kuanzia mwaka 2011 hadi 2016.

Taarifa ya uteuzi huo imetangazwa leo Mei 27, 2026 sambamba na mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa ndani ya Serikali ya Uganda ambapo baadhi ya mawaziri wa muda mrefu wameondolewa huku wengine wakibaki katika nafasi zao.

Katika Baraza hilo jipya, Jessica Alupo ameendelea kubaki kama Makamu wa Rais huku Robinah Nabbanja akiendelea kushika nafasi ya Waziri Mkuu.

Hata hivyo, aliyekuwa Waziri wa Fedha Matia Kasaija pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa muda mrefu Moses Ali hawajarejea katika Baraza hilo jipya.

Uteuzi huo unaendelea kuonyesha nafasi kubwa ya Janet Museveni ndani ya Serikali ya Uganda ambapo ameendelea kuwa mmoja wa viongozi waliodumu kwa muda mrefu katika Baraza la Mawaziri la nchi hiyo.

Leave a Comment