×

Aliyekuwa Mchezaji Wa Southampton Afariki Akiwa Na Miaka 21

Klabu ya Southampton F.C. pamoja na Royal Antwerp F.C. zimethibitisha kifo cha aliyekuwa mchezaji wao wa akademi, Victor Udoh aliyefariki akiwa na umri wa miaka 21.

Udoh alitumia miezi sita katika akademi ya Southampton kuanzia Februari 2025 ambapo alicheza michezo minane kwa kikosi cha vijana chini ya miaka 21 katika mashindano ya Premier League 2.

Kabla ya kuhamia England, winga huyo kutoka Nigeria alikuwa sehemu ya akademi ya Royal Antwerp nchini Belgium na alifanikiwa kucheza mechi 28 akiwa na kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Baada ya kuondoka Southampton mwezi Septemba mwaka jana, Udoh alijiunga na klabu ya daraja la pili nchini Czech Republic, SK Dynamo České Budějovice.

Kupitia ukurasa wao wa X, Southampton walisema wameumizwa na taarifa za kifo hicho huku wakitoa pole kwa familia na wapendwa wa mchezaji huyo.

Nayo Royal Antwerp ilieleza kushtushwa na taarifa hizo na kusisitiza kuwa mawazo yao yako pamoja na familia, marafiki na watu wa karibu wa Victor Udoh katika kipindi hiki kigumu.

BODABODA AJIRUSHA ILI AKANYAGWE na LORI DARAJA la UBUNGO – TAIRI LAMKANYAGA na KUFARIKI PAPO HAPO…

Leave a Comment