
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Emmanuel Nchimbi amefika katika Viwanja vya Kilimani vilivyopo Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita kwa ajili ya kushiriki Ibada ya kumuaga na kumuombea Marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli.
Ibada hiyo inayofanyika leo Mei 29, 2026 imewakutanisha viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu, jamaa pamoja na wananchi waliofika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu ambaye alikuwa Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli.

Mhe. Nchimbi ameungana na waombolezaji wengine katika shughuli hiyo ya maombi na kuaga mwili wa marehemu kabla ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika Chato mkoani Geita.
Bi. Suzana Ngolo Magufuli anakumbukwa kwa malezi na mchango wake mkubwa kwa familia pamoja na jamii inayomzunguka.



