
Kampuni ya Meridianbet imeonesha tena moyo wa kijamii kwa kutoa msaada wa vyandarua maalumu kwa Hospitali ya Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mabwepande, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono huduma bora za afya kwa wananchi.
Tukio hilo limeonesha wazi kuwa Meridianbet haipo tu kwenye ulimwengu wa burudani, bali pia ni daraja la matumaini kwa jamii. Msaada huo umelenga kuboresha mazingira ya wagonjwa wodini na kuhakikisha wanapata huduma katika hali yenye faraja na usafi zaidi.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Habari wa kampuni, Nancy Ingram, alieleza kuwa Meridianbet imejenga utamaduni imara wa kusaidia jamii. Alisisitiza kuwa dhamira yao ni kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi, hasa katika sekta nyeti ya afya ambayo inagusa maisha ya kila mtu.
Uongozi wa Hospitali ya Mabwepande ulipokea msaada huo kwa furaha na shukrani kubwa, ukibainisha kuwa vyandarua hivyo vitakuwa msaada muhimu katika kuboresha huduma za wodi. Wameeleza kuwa hatua hiyo imeleta nafuu na kuongeza ubora wa mazingira ya matibabu kwa wagonjwa.
Kwa miaka kadhaa sasa, Meridianbet imeendelea kuwekeza katika miradi ya CSR, ikisaidia shule, vituo vya watoto yatima na hospitali mbalimbali. Hii inaonesha kuwa kwao, mafanikio ya biashara yanakwenda sambamba na kugusa maisha ya watu na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.