×

Mama Alia Mbele ya Waziri Mkuu Akidai Mwanaye Kuchukuliwa na Wanaojiita Polisi – Video

Kumetokea tukio la kusikitisha ambapo mama mmoja ameonekana akiomba msaada mbele ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, akidai kuwa mwanaye alichukuliwa kienyeji na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa polisi.

Mama huyo ameonekana akieleza kwa uchungu mkubwa tukio hilo, akitaka mamlaka husika kulifuatilia na kumpatia haki kuhusu kilichotokea kwa mtoto wake.

Tukio hilo limeibua hisia kali miongoni mwa wananchi waliokuwepo, huku likizidi kuibua mjadala kuhusu usalama na utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya vyombo vya dola.

Leave a Comment