×

Video: Makonda Awaomba Watanzania Kuwapa Morali Serengeti Boys

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anawatunza, anawalea na kuwapa morali vijana wa timu ya Serengeti Boys ili waendelee kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Makonda amesema mafanikio ya Serengeti Boys si mafanikio ya timu pekee, bali ni ushindi wa Watanzania wote, hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa jamii kuendelea kuwaunga mkono vijana hao katika safari yao ya soka.

Amesisitiza kuwa vijana hao wanahitaji mazingira bora, sapoti na hamasa kutoka kwa Watanzania ili kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa katika michuano ya kimataifa.

Leave a Comment