×

Video: Dada wa Mtanzania wa Aliyekamatwa Oman Afunguka Mazito Global TV

Dada wa Mtanzania, Ashura Abdul Salum, amezungumza na Global TV kupitia kipindi cha #Mapito na kueleza hali ya mdogo wake Hidaya Abdul Salum ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi nchini Oman kwa tuhuma za wizi wa mkufu.

Ashura amesema familia yao imekuwa na sintofahamu kutokana na maelezo yanayotolewa na washtaki, ambao ni waliokuwa waajiri wa Hidaya, akidai kuwa taarifa hizo zimekuwa zikitofautiana na hivyo kuzua mashaka kuhusu ukweli wa tuhuma zinazomkabili mdogo wake huyo.

Ameeleza kuwa Hidaya amekaa rumande kwa takribani mwezi mmoja sasa, huku familia ikiendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo na kutafuta ufafanuzi zaidi kuhusu hatma yake.

Familia hiyo imesisitiza kuwa ina wasiwasi mkubwa na inatumai suala hilo litafanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa kilichotokea.

Leave a Comment