×

Exclusive: Mchungaji Msigwa Afichua Mazito, Sababu Kurudi Chadema Tume Ya Chande -Video

Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo aliyerejea ndani ya chama hicho baada ya awali kuhamia CCM, Peter Msigwa amesema hali ya kisiasa nchini Tanzania kwa sasa haifurahishi, akieleza kuwa matukio yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 yalichangia kufanya tafakari kubwa kuhusu mustakabali wake wa kisiasa.

Msigwa, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema kwa vipindi viwili, alitangaza kurejea Chadema Mei 2026 baada ya kukaa ndani ya CCM kwa takribani miaka miwili. Katika maelezo yake, alisema hawezi kuendelea “kuishi kwa huzuni na ukimya,” akisisitiza kuwa dhamira yake imemrudisha upande anaoamini una ukweli na haki.

Aidha, Msigwa alifichua kuwa swali kutoka kwa mwanawe mwenye umri wa miaka 18 lilikuwa moja ya vitu vilivyomsukuma kufanya uamuzi wa kurejea Chadema, huku akieleza kuwa alitumia miezi kadhaa kutafakari kuhusu mwenendo wa siasa nchini pamoja na taarifa za mauaji na matukio ya vurugu yaliyoripotiwa baada ya uchaguzi.

Leave a Comment