
Sakata limeibuka ndani ya Familia ya Kifalme ya Uingereza kati ya Prince William na Queen Camilla kufuatia maandalizi ya harusi ya Peter Phillips.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mvutano huo unahusiana na suala la mavazi ya kifalme, hususan kama bibi harusi mtarajiwa, Harriet Sperling, ataruhusiwa kuvaa tiara siku ya harusi yake.
Inadaiwa kuwa ofisi ya Camilla ilizuia matumizi ya vito kutoka kwenye hazina ya kifalme kwa watu wasio wa damu ya kifalme, jambo lililozua kutokubaliana ndani ya familia. Hata hivyo, inaripotiwa kuwa William alipingana na uamuzi huo na kuingilia kati, hatua iliyosababisha kile kilichoelezwa kama “mvutano mkali” ndani ya familia ya kifalme.

Harusi hiyo inatarajiwa kufanyika Juni 6 na itahudhuriwa na baadhi ya wanachama wa familia ya kifalme, ingawa baadhi ya wahusika wakuu kama Prince Harry na Meghan Markle hawatarajiwi kuwepo.
Sakata hilo limezidi kuchochea gumzo nchini Uingereza, huku wachambuzi wa mambo ya kifalme wakisema linaonyesha mvutano mdogo unaoendelea ndani ya familia hiyo maarufu duniani.