×

Ronaldo Kuongoza Kizazi cha Wachezaji Wakongwe Marekani 2026

Wachezaji saba wenye umri wa miaka 40 na zaidi wanatarajiwa kushiriki kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026, jambo linaloonyesha uimara na maisha marefu ya soka kwa baadhi ya nyota wakubwa duniani.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Cristiano Ronaldo ambaye akiwa na miaka 41 anatarajiwa kuweka historia kwa kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya sita.

Golikipa wa Scotland, Craig Gordon, ndiye atakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwenye mashindano hayo akiwa na miaka 43.

Wengine wanaotarajiwa kushiriki ni Luka Modrić wa Croatia, Manuel Neuer wa Ujerumani, Edin Džeko wa Bosnia na Herzegovina pamoja na Guillermo Ochoa wa Mexico ambaye pia anatarajiwa kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya sita.

Aidha, golikipa Vozinha wa Cape Verde naye anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho katika ushiriki wa kwanza wa taifa hilo kwenye Kombe la Dunia.

Leave a Comment