×

TAMISEMI Yatangaza Nafasi 400 za Walimu wa Biashara, Mwisho wa Maombi Juni 14, 2026

TAMISEMI imetangaza nafasi 400 za walimu wa kujitolea (mkataba) kwa somo la Elimu ya Biashara katika shule za sekondari zenye uhitaji mkubwa wa walimu.

Ajira hizo zinatekelezwa kwa ushirikiano na Educate! Tanzania kupitia mradi wa kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Business Studies.

Soma zaidi hapa AJIRA ZA MKATABA WALIMU WA SOMO LA BIASHARA

Mikoa yenye nafasi

Nafasi hizo zinapatikana katika mikoa ya:

  • Arusha Region
  • Kilimanjaro Region
  • Manyara Region
  • Simiyu Region
  • Kagera Region
  • Geita Region
  • Tabora Region
  • Dodoma Region
  • Morogoro Region
  • Pwani Region
  • Dar es Salaam

Sifa za waombaji

Waombaji wanatakiwa kuwa:

  • Raia wa Tanzania
  • Mwenye umri usiozidi miaka 42
  • Mwenye Shahada inayohusiana na Biashara au Uchumi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

Fani zinazokubalika ni pamoja na:

  • Bachelor of Education in Business Studies / Business Education
  • Bachelor of Commerce (BCom)
  • Bachelor of Business Administration (BBA)
  • Bachelor of Economics / BA in Economics
  • Shahada nyingine zinazohusiana na biashara

Pia mwombaji anatakiwa:

  • Kuwa na uwezo wa kutumia kompyuta
  • Asiwe mwajiriwa wa Serikali au taasisi nyingine
  • Awe na NIDA
  • Kuambatisha vyeti vyote muhimu pamoja na barua ya maombi

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yanapaswa kutumwa kupitia mfumo rasmi wa ajira wa TAMISEMI:

Mfumo wa Ajira TAMISEMI

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14 Juni 2026 saa 05:59 usiku.

Soma zaidi hapa AJIRA ZA MKATABA WALIMU WA SOMO LA BIASHARA

Leave a Comment