×

Rais Samia Arejea Tanzania Kutoka Ziara ya Urusi, Makamu wa Rais Ampokea (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MDkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais  Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 06 Juni, 2026 baada ya kuhitimisha Ziara yake ya Kitaifa, St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026 kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Vladmir Putin.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amerejea nchini leo Juni 6, 2026 akitokea jijini St. Petersburg nchini Urusi alipokuwa katika ziara ya kitaifa ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, Rais Samia alipokelewa na Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel John Nchimbi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro na viongozi wengine wa Serikali na chama.

Akiwa nchini Urusi, Rais Samia alishiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF) pamoja na kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na viongozi mbalimbali kuhusu ushirikiano wa kiuchumi, biashara, uwekezaji na maendeleo kati ya Tanzania na Urusi.

Ziara hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya juhudi za Tanzania kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali muhimu ikiwemo nishati, miundombinu, utalii na biashara.

Leave a Comment