×

Waziri wa Mambo ya Nje Iran Amjibu Rais wa Lebanon Kwa Maneno Makali

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi.

TEHRAN, Iran — Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa kauli kali akimjibu Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, kufuatia ukosoaji wake dhidi ya Iran kuhusu madai ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye mtandao wa X siku ya Jumamosi, Araghchi alisema kuwa kauli za Rais Aoun zinaweza kuwafanya watu waamini kwamba Iran ndiyo inayohusika na uharibifu au mzozo unaoikumba Lebanon, akikanusha vikali tuhuma hizo.

Alikwenda mbali zaidi kwa kuishauri Lebanon ijilinde na adui wake wa kweli, akisisitiza kuwa matatizo ya nchi hiyo hayapaswi kuelekezwa kwa Iran.

Rais wa Lebanon, Joseph Aoun

Kauli hiyo imekuja kufuatia mahojiano ya Rais Joseph Aoun na CNN, ambapo aliitaka Iran kutoingilia masuala ya ndani ya Lebanon na kuheshimu mamlaka ya nchi hiyo.

Mvutano huu mpya unaongeza joto katika uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tehran na Beirut, ambao mara kwa mara umekuwa ukikumbwa na tofauti za kisiasa na kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

Leave a Comment