
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa jumla ya shahada nane za heshima (Honorary Doctorates) tangu alipoingia madarakani mwaka 2021. Shahada hizo zimetolewa na vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kwa kutambua mchango wake katika uongozi, diplomasia, elimu, utalii, uchumi na maendeleo ya kijamii.


Hizi ni shahada za heshima alizotunukiwa:
- University of Dar es Salaam – Doctor of Letters (D.Litt) Honoris Causa (2022)
Alitunukiwa kwa mchango wake katika elimu, haki za binadamu na maendeleo ya Tanzania. - Jawaharlal Nehru University – Doctor of Philosophy (Honoris Causa) (2023)
Kwa kuimarisha uhusiano kati ya India na Tanzania pamoja na diplomasia ya uchumi. - State University of Zanzibar – Doctor of Philosophy in Tourism Management and Marketing (Honoris Causa) (2023)
Kwa mchango wake mkubwa katika kukuza utalii kupitia kampeni ya Royal Tour. - Ankara University – Honorary Doctorate in Economics (2024)
Kwa uongozi wake katika mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. - Korea Aerospace University – Doctor of Philosophy in Aviation Management (Honoris Causa) (2024)
Kwa mchango wake katika maendeleo ya sekta ya anga Tanzania. - Mzumbe University – Honorary Doctorate in Leadership (2024)
Kwa uongozi wake na mchango katika maendeleo ya taifa. - Nasarawa State University – Doctor of Letters (Honoris Causa) (2026)
Kwa mchango wake katika uwazi, uwajibikaji, uwezeshaji wanawake na maendeleo ya uchumi. - Peoples’ Friendship University of Russia (RUDN) – Honorary Doctorate (Honoris Causa) (2026)
Kwa mchango wake katika elimu, diplomasia na kuitangaza Tanzania kimataifa.
