
Mwanamama Salome Lawrance Kikoti ambaye siku chache zilizopita alitrend kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufanya tukio la aina yake, la kuzuia kijana aliyekuwa anataka kuuawa na wananchi wenye hasira kali, ametokwa na machozi ya furaha baada ya Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo kutimiza ahadi yake kwake.
Baada ya kuiona video hiyo, Shigongo alituma ujumbe akimtaka mama huyo kuwasiliana na meneja wa tawi lolote la Benki ya CRDB ili amtumie ‘sadaka’ yake, jambo ambalo amelitimiza.
Baada ya kupokea ‘sadaka’ kutoka kwa Shigongo, mama huyo akashindwa kujizuia kumwaga machozi, akimshukuru Mungu kwa muujiza aliomfanyia.