
Mwili wa Meneja wa Mipango na Fedha wa kampuni ya MATI Super Brands Limited, Goodluck Didas Silayo, utaagwa leo Juni 16, 2026 nyumbani kwake mtaa wa Komoto, Babati na utazikwa katika eneo la Babati Day, Manyara.
Silayo alifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Juni 12, 2026 katika eneo la Chenene, Mkoa wa Dodoma. Taarifa zilizotolewa zinaeleza kuwa alikuwa akiendesha gari lake lililogongana na lori la Semitrailer majira ya saa 2:00 usiku, na kufariki papo hapo katika eneo la tukio.

Akizungumzia msiba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa MATI Super Brands Limited, David Damian Mulokozi, amesema kifo cha Silayo ni pigo kubwa kwa familia, kampuni pamoja na jamii kwa ujumla kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taasisi hiyo.
Mulokozi amesema marehemu alikuwa mtumishi mwenye weledi, uaminifu na kujitolea katika kutekeleza majukumu yake, na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya biashara na maendeleo ya kampuni.




