×

Kajala Amtembelea Wema Baada ya Kujifungua, Wafufua Urafiki

Staa wa filamu, Kajala Masanja (kushoto) akiwa na Wema Sepetu

Baada ya muda mrefu takribani miaka mitano wakiwa hawako karibu, mastaa wa filamu Tanzania, Kajala Masanja na Wema Sepetu hatimaye wameonekana kurejesha ukaribu wao wa zamani.

Uhusiano huo mpya umeonekana baada ya Kajala kumtembelea Wema hivi karibuni, hatua iliyofuatia furaha ya Wema kupata mtoto, jambo lililopokelewa kwa hisia nzuri na mashabiki wengi.

Kwa muda wa zaidi ya miaka mitano, wawili hao walikuwa na tofauti zilizowafanya waepukane, huku chanzo chake kikihusishwa na sintofahamu zilizowahi kuhusisha masuala ya mapenzi. Hata hivyo, sasa inaonekana pande zote zimeamua kuweka kando tofauti hizo na kuanza ukurasa mpya wa amani na urafiki.

Mashabiki wamefurahia hatua hiyo, wakisema ni moja ya maridhiano makubwa zaidi katika tasnia ya filamu Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.

KAULI za UBAGUZI BUNGENI! MUSUKUMA AKINUKISHA – “SISI HATUMJUI MZANZIBARI – RAIS CHUKUA HATUA”

Leave a Comment