×

Kauli ya Paula Kajala Yawaacha Mashabiki na Maswali Mitandaoni

Paul Kajala akiwa na mpenzi wake Omary Mwanga almaarufu Marioo.

Mrembo na staa wa mitandao ya kijamii, Paula Kajala, amewavutia mashabiki wake baada ya kushiriki ujumbe wenye mafunzo kuhusu mahusiano na uchaguzi wa mtu wa kuwa naye maishani.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Paula aliandika: “Hifadhi moyo wako kwa mtu anayekuletea amani katika maisha yako, si machafuko.” (Save your heart for someone who adds peace to your world, not confusion)

Tafsiri yake ikiwa ni:

Ujumbe huo umeibua hisia na tafsiri tofauti kutoka kwa wafuasi wake, huku baadhi wakiamini kuwa ni ushauri wa kawaida wa maisha na mahusiano, wakati wengine wakihusisha na hali yake binafsi.

Hata hivyo, Paula hakutoa maelezo zaidi kuhusu alichomaanisha, jambo lililowaacha mashabiki wake wakijadili ujumbe huo kwa mitazamo mbalimbali.

Leave a Comment