×

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba Asafiri kwa SGR Kutoka Dodoma hadi Dar – Picha

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, leo Alhamisi Juni 18, 2026, amesafiri kwa treni ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli za kikazi.

Katika safari hiyo, Waziri Mkuu ameambatana na Mwenza wake, Mama Neema Mwigulu Nchemba, ambapo walitumia huduma ya reli hiyo ya kisasa inayounganisha miji mbalimbali nchini na kurahisisha usafiri wa abiria na mizigo.

Safari ya Dkt. Nchemba kupitia SGR inaendelea kuonyesha matumizi ya miundombinu ya kisasa ya reli iliyojengwa na Serikali kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri, kuongeza ufanisi wa safari na kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini.

TRUMP na RAIS wa IRAN WASAINI HATI ya MAKUBALIANO ya KUSITISHA MAPIGANO – IRAN vs ISRAEL….

Leave a Comment